Abu Hamza, msemaji rasmi wa Saraya al-Quds, tawi la kijeshi la Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina, amesema: "Iwapo utawala wa Israel hautasimamisha mashambulizi yake ya kikatili, hatima ya mateka hawa ambao tunawashikilia itakuwa kama ya Ron Arad ambaye hajasikika kwa zaidi ya miaka 40.
Afisa huyo wa kijeshi wa wanamapambano wa Saraya al-Quds amesema, adui Mzayuni anaendelea kuua watoto, wazee na wanawake bila ya kujali lolote, akidai kuwa mauaji hayo ni kujibu juhudi zetu ambazo kimsingi zinapigania uhuru wetu na kutaka kuondoka katika makucha ya utawala wa Kizayunii wa Israel unaozikalia kwa mabavu ardhi zetu.
Hayo yanajiri katika halii ambayo, duru za hospitali za Palestina zilitangaza jana usiku juu ya kuongezeka idadi ya mashahidi wa mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kuthibitisha kuwa, hadi sasa watu 687 wameuawa shahidi.Wizara ya Afya ya Palestina yenye makao yake makuu katika Ukanda wa Gaza pia ilitangaza kuwa, 140 kati yao ni watoto na 105 ni wanawake. Mapigano kati ya wapigania ukombozi wa Palestina na jeshi la utawala vamizi wa Israel yameendelea leo kwa siku ya nne katika maeneo ya ndani ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni karibu na Ukanda wa Gaza, ukiwa ni mwendelezo wa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyoanzishwa na Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Hamas) dhidi ya uvamizi wa Israeli, huku kukiwa na makadirio kwamba Wazayuni wasiopunguau 1,000 wa Israeli wameangamizwa hadi sasa.
342/